Saturday, December 24, 2011

Qudus English Medium Primary School yashinda vizuri katika Manispaa ya Bukoba.

Qudus English Medium Primary School yashinda vizuri katika matokeo ya mtihani wa darasa la nne ndani ya manispaa ya Bukoba ambapo kuna shule binafsi za mfumo wa kiingereza na kiswahili nkongwe na zenye mbinu kabambe za ufunishaji imekuwa shule ya tatu. Shule hii yenye kumilikuwa na waislamu ni mpya na huu ndo ulikuwa mtihani wa kwanza wa kitaifa hii shule changa kuufanya lakini Mungu ni mkubwa shule hii imeshinda vizuri na watoto wote wana Alama za "A". Sheikh Musa Abeid ambaye ni mwalimu pale na imamu wa msikiti Markaz Kashai amesema baada ya sala ya Alfajiri kuwa wanafunzi wote wamepata "A" na kumshukuru Allah(SW) na kuwashukuru walimu wanaofundisha kwa moyo wa kujituma wakiwa na Mwalimu Mkuu mzoefu Mwalimu Elias Kateme, huyo mwalimu akiwa na timu yake ya walimu hawana budi kushukuru Allah ili aongeze ufanisi kutokana na juhudi zao ili hatimaye mitihani ijayo wawe wa kwanza Insha Allah.

Sasa na la saba imepata A nyingi na B+ tu, jamani tuwaunge mkono viongozi wa Shule hii na Allah atawasaidia na kuwapa hekima zaidi na subira kwani kuongoza shule za jamii ni kazi.

2 comments:

  1. Naomba kupewa mawasiliano ya mkuu wa shuke ya Qudus pre and primary school ili anifafanulie utaratibu wa kusajili mtoto wangu hapo. Jina langu Idrisa nipo Musoma. Ahsante.

    ReplyDelete
  2. Naomba kupewa mawasiliano ya mkuu wa shuke ya Qudus pre and primary school ili anifafanulie utaratibu wa kusajili mtoto wangu hapo. Jina langu Idrisa nipo Musoma. Ahsante.

    ReplyDelete

CHANGIA MAWAZO YAKO/USHAURI KWA MANUFAA YA JAMII. UNA MAWAZO YAKO NA YANAWEZA KUWA NA MANUFAA YATOE TAFADHALI. KARIBU SANA