Saturday, December 3, 2011

Hotuba ya Ijumaa Msikiti wa Bilele(Uswahilini) Bukoba Tanzania Tar.25/11/2011

Sheikh Haruna Kichwabuta ambaye ni Sheikh wa Wilaya ya Bukoba Manispaa, alianza hutuba ya ijumaa takriban saa 7.05 za mchana wa siku ya Ijumaa. Alianza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu(SW) na Kumtakia rehema na Amani Mtume wake. Waislam walipewe ujumbe wa kumcha Mwenyezi Mungu na Kufuata mwenendo wa Mtume wetu Muhammad(SAW). Sheikh Haruna Kichwabuta aligusia harakati za Mtume akiwa Maka na kuanza kutangaza Mungu mmoja Allah(SW) na vipingamizi alivyopata katika harakati hizo kutoka kwa Makuraishi washirikina, Sheikh Haruna kichwabuta aligusia safari ya kuhama kwa siri kwa mtume na baadhi ya maswahaba kwenda Madina(Hejira), alisema walikwenda na Abubakar huku wakifuatiliwa na Makafiri ili wawakamate na wawauwe huku aliyebaki kwenye kitanda cha mtume alikuwa Saidina Ali na baadaye Mtume aliingia pangoni kujificha na Saidina Abubakari, Sheikh Haruna Kichwabuta alisema Abubakari aliingia kwanza pangoni na kusafisha ili kucheki usalama pangoni ili mtume asizulike kwanza, katika hili alilauma Mtunzi wa kitabu kimoja nchini Tanzania aliyesema kuwa saidina Abubakari pale pangoni hakuwa na umuhimu wowote na yule mtunzi wa kitabu akamfananisha na Mbwa aliyekuwa amejinyosha kwenye lango la vijana wa pangoni. Hii Sheikh Haruna Kichwabuta alilaumu upotoshaji wa mtunzi wa kitabu hicho na kusema Saidina Abubakari walikuwa na Mtume kwenye harakati na pangoni aliingia Abubakari kwanza kuangalia usalama wa pango!
Sheikh Haruna Kichwabuta alisisitiza kujitahidi kufanya mambo ya kheri ili kupata radhi za Allah(SW) na kujitahidi kufanya maendeleo kwa ajili yetu wenyewe na kusomesha watoto elimu ya dini na elimu zinginezo

No comments:

Post a Comment

CHANGIA MAWAZO YAKO/USHAURI KWA MANUFAA YA JAMII. UNA MAWAZO YAKO NA YANAWEZA KUWA NA MANUFAA YATOE TAFADHALI. KARIBU SANA