Tunapenda kuwaomba walimu wa dini waige mfano wa Mwalimu wa Qudus English Medium Primary School ya Bukoba Tanzania kuelimisha watu wazima wanaotaka kusoma uislamu. Darasa hili lakaribia kumaliza mwaka tangia lianze na sasa kinachoombwa ni kuwahimiza watu wazima wasome uislamu vizuri bila kusingizia umri na majukumu kwani kujua uislamu wako ni jambo la kwanza ili ufuate uislamu unaojua na sio wa kuzaliwa na kuigiza waislamu wengine bila kusoma wewe mwenyewe. Katika uislamu elimu haina mwisho na ni wajibu wa kila muislamu kusoma mpaka anaingia mwanandani yaani kaburini.
Tumuombee Mwalimu Twaibu Hussein asikate tamaa katika kuendeleza darasa la watu wazima hapa Msikitini Kashai Markaz na Allah atamlipa hapa duniani na Kesho Akhera Insha Allah.

WhatsApp :+255621870342. Muabudu Mungu mmoja wa Pekee na hana mshirika, Hakuna Mtume aliyetumwa kama Mungu wala Mwana wa Mungu. (Qur'ani) Al Imran 3.31,Yohana 7.16-18. Shetani na kundi lake miongoni mwa wanadamu amejizatiti kuwapotosha watu kupitia shida mbali mbali. Imani kuhusu Mungu mmoja wa pekee ndo suluhisho la kudumu na kuishi na matumaini hapa duniani. Wasiliana nasi upate ushauri na tiba WhatsApp :+255621870342, Email: tibaherbs@gmail.com, +255 762053174
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
CHANGIA MAWAZO YAKO/USHAURI KWA MANUFAA YA JAMII. UNA MAWAZO YAKO NA YANAWEZA KUWA NA MANUFAA YATOE TAFADHALI. KARIBU SANA