Hotuba hii imetolewa na Sheikh Yusufu Kakwekwe na ni mwalimu Nyanshenye Sekondari ambayo shule iko chini ya Taasisi ya Kiislam iitwayo Bukoba Islamic Centre. Sheikh Kakwekwe pia ni Mwalimu Mkuu wa masomo ya dini katika madrasat Fauzu katika Manispaa ya Bukoba Tanzania.
Sheik Yusufu Kakwekwe alianza kwa kumhimidi Allah(SW) na kumsalia Mtume wetu, kisha kuwakumbusha waislam kumcha Allah(SW) na kuelezea mwezi tuliomo kuwa ni wa kwanza katika miezi ya kiislam na akasisitiza kusaidia wajane, mayatima, maskini na kuchangia maendeleo ya kiislam kwani mali ya mtu itakuwa yenye kuulizwa siku ya kiama namna ulivyoipata na matumizi yake. Kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu alinukuu aya za Qur'an na akaelezea umuhimu wake kwa wale wenye mali, alisema usikalie mali yako kwani ALLAH ndo mtoaji na inabidi tutoe zaka na sadaka sitahiki kadiri ya uwezo wa kila muislamu.
Amesisitiza waislam tutumie umri wetu kufanya mema na siyo kuendelea kufanya mabaya kama kudhulumu, kufanya ufisadi, kuzuru watu na akasema tupo bado tutoe toba na tufanye mema.
Sheikh Yusufu Kakwekwe alisema watu wenye ujuzi wautumie ujuzi wao kwa manufaa ya jamii na wakiutumia vibaya wataulizwa kwani Allah amewapa kama Amana na inabidi wasiutumie kuzuru watu na kufanya ufisadi katika ardhi

WhatsApp :+255621870342. Muabudu Mungu mmoja wa Pekee na hana mshirika, Hakuna Mtume aliyetumwa kama Mungu wala Mwana wa Mungu. (Qur'ani) Al Imran 3.31,Yohana 7.16-18. Shetani na kundi lake miongoni mwa wanadamu amejizatiti kuwapotosha watu kupitia shida mbali mbali. Imani kuhusu Mungu mmoja wa pekee ndo suluhisho la kudumu na kuishi na matumaini hapa duniani. Wasiliana nasi upate ushauri na tiba WhatsApp :+255621870342, Email: tibaherbs@gmail.com, +255 762053174
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
CHANGIA MAWAZO YAKO/USHAURI KWA MANUFAA YA JAMII. UNA MAWAZO YAKO NA YANAWEZA KUWA NA MANUFAA YATOE TAFADHALI. KARIBU SANA