Monday, December 19, 2011

Wanawake wa Kiislamu Bukoba chini ya Baraza kuu la waislamu Tanzania waazimia kujenga Hospitali ya Wanawake na Watoto

Hii ni habari njema kuona wanawake wakiislamu mjini Bukoba wameamua kuanzisha mchakato wa ujengaji Hospitali kwa ajili ya wanawake na watoto ili kutimiza wajibu mojawapo ya kijamii na kuwaeleza watu wenye kuwaunga mkono wawaunge mkono wa kimawazo, hali na mali ili watimize mpango wao huu mzuri.
Insha Allah tunaomba muwaunge mkono ili Hospitali isimame na Allah atalipa kila juhudi ya mtu kwani afya ni jambo la msingi na bila afya mambo yote yanakwama na hayafanyiki kwa ufanisi kwani hata mtume wetu alikuwa anaomba Allah amjalie afya ili aweze kufanya ibada na amali mbalimbali. Kwa hiyo hawa wakina mama wamegusa kitengo muhimu cha kuwezesha waislamu na watu wengine wapate huduma ya afya na hatimae wawe na nguvu za kufanya mambo mengine ya kijamii na kumcha Allah ipasavyo.

2 comments:

  1. Assalaam alaykum warahmatullah wabarakatuh.

    Juhudi ya kujenga hospitali ya wanawake na watoto inayofanywa na kikundi cha akina mama kwa kushirikiana na baadhi ya wanaume hapa Bukoba mjini ni jambo adhimu mno. Kufanikiwa kwa juhudi hii kutakuwa ni Ukombozi wa mwanamke wa kiislam.

    Kwa sasa wanawake walio wengi zaidi wanakwenda kujifungua katika hospitali ya Mugana, ambayo ukiacha kuwa wanahudumiwa na wanaume (daktari mkuu) bado kila kitanda kina masananu ya Bikira Maria, nk

    Ikumbukwe kuwa Uislam unamheshimu na kumthamini sana mwanamke hata ukamlazimisha kuvaa stara ili asipate kusumbuliwa. Hatahivyo, kwa muda mrefu wanawake wamekuwa wakijistiri lakini ikifika wakati wa kujifungua wanajikuta wakilazimika kuwavulia wanaume (na mbaya zaidi wasiokuwa waisalam) ili wawahudumie. Kitendo hiki ni udhalilishaji mkubwa kwa heshima ya maumbile ya mwanamke na hisia zake.

    Ninachoweza kushauri hapa ni kwamba tunatakiwa kuunga mkono juhudi hii kwa hali na mali. Lakini zaidi ya yote tusisahau kuwaandaa wataalam (Doctors, nurses, phisicians) watakaotoa huduma katika hosptali hiyo.

    Ni muhimu kukumbuka kuwa mafunzo ya udaktari huchukua muda mrefu (miaka mitano), hivyo hatuna budi kujipanga mapema ili isije ikatokea tukajenga hospitali kisha ikakosa wahudumu na hivyo kupelekea hata wanawwake wwa kiislam kuikimbia na kuipiga vijembe.

    Mwisho, mi nadhani mbinu bora zaidi ya kuandaa wataalam ni kutafiti wasichana wa kiislam walioko katika Vyuo (wanaosomea udaktari na madawa) pamoja na wanaosoma michepuo ya sayansi (PCB, CBG, PCM, CBA, PGM)ili tubaini ni nani na nani yuko tayari kuwasaidia wanawake wenzake kwa ajili ya Allah ili 'tuwawezeshe' na kuwatanabaisha juu ya wajibu wao katika Uislam. Kuwawezesha ni lazima, kwani masomo hayo ni magumu wanahitaji kusoma Tuitions, na kununua vitabu na mahitaji mengine na kwammba kuwawezesha ni motisha kwao.

    Ni muhimu kudokeza pia, kuwa hata wanawake wasiokuwa wa kiislam watahitaji kuhudumiwa katika hospitali hiyo, kwa sababu hakuna mwanamke mwenye akili ambaye angependa kumvulia nguo mwannamume asiye mume wake ili ampime au amsaidie kujifungua.

    Allah atuwekee wepesi katika juhudi hii.

    Sadam Matsawili J.K

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asalam Aleikum Sadam Matsawil. ahsante kwa kuchangia mada muhimu na kutoa mikakati na dira. Allah akuzidishie upeo na uwezo kielimu na kiuchumu ili usaidie uislam kwa nafsi na mali.

      Delete

CHANGIA MAWAZO YAKO/USHAURI KWA MANUFAA YA JAMII. UNA MAWAZO YAKO NA YANAWEZA KUWA NA MANUFAA YATOE TAFADHALI. KARIBU SANA