Mwalimu Atwibu Hussein baada ya sala ya Ishah alimkaribisha mgeni ajitambulishe kwa waisalmu, mgeni alikuwa safarini kuelekea Karagwe kwa ajili ya mazishi ya mwanafunzi wa Kirinjiko aliyeaga duniani, inna llillah waina ileiy rajiuun.
Mgeni alijitambulisha kwa jina Imrani Atibu na Mwalimu Kirinjiko Islamic Centre, Mwalimu Imran Atibu ameongelea mambo kuhusu hali ya sasa na waislamu wa sasa kama kuiga mambo ya kimagharibi na kuacha kujifunza uislamu wetu vizuri na kufuata mbinu za Mtume wetu katika kueneza kalima na kuamsha waislamu ili waweze kujua wajibu wao na kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa mafundisho ya uislamu.
Amesema waislamu tuko wavivu wa kusoma na hatutaki kusoma uislamu na kuujua vizuri, hii itatusaidia kupunguza mitafaruku miongoni mwetu kwani watu waliosoma dini vizuri na kufuata mafundisho si rahisi kugombana na kutoelewana kama tunavyoona hivi sasa. Maadili yameharibika mpaka sasa tunaona duniani inavyochafuka kiasi kwamba mtu anataona heri ya jana kila kukicha. Mwalimu Imran Atibu amesema mpaka sasa nchi za ulaya zimelazimisha nchi maskini zikubali wanaume kuoa wanaume wenzao wakitaka ndipo zitapewa misaada ya kiuchumi hii inaonyesha duniani inavyoelekea pabaya kiasi kwamba mtu mchamungu kweli hatapata raha dunia ya sasa ila atakaa katika huzuni n hii inathibitisha maneno ya Mtume aliposema itafika zama muumini atamani kuwa kaburini kuliko kuishi duniani kwa mambo yatakavyochafuka.
Mwalimu Imrani Atibu ameelezea ujanja wa kupamba mambo ya kupotosha na kuyafanya kuwa kama halali kwa waislamu wa kawaida kama kuanzishwa Islamic Banking inavyopaliliwa kwa waislamu ili waweke pesa yao na Benki zifanyie biashara kwa kukopa watu wengine na kupata riba na wewe muislamu ukitaka pesa yako wanakupa bila riba na huku wamezitumia katika biashara ya kukopa kwa riba na pesa yako imeshirika katika biashara haramu ya riba na wewe unaaambiwa ni Islamic Banking. Mwalimu amesema pesa yako ni bora uifanyishe biashara ili izae faida halali na uajiri watu wengine nao wapate faida na hatimae umaskini upungue kwenye jamii.Kwa mfumu wa kiislamu ni kushirikiana katika faida na hasara na siyo hasara kwa upande mmoja tu wa mteja au faida kwa mteja tu, hii iwe sawa ni mpaka upate mkopo bila riba na kama ni biashara mugawane kwa hali ya faida au hasara ndio utaratibu sahihi wa kiislamu katika mfumo wa uchumi, uislamu unazuia kurundika mali bila kuitumia kuzalisha na kutoa dhaka na sadaka ili jamii iwe na maisha bora, ametoa mfano wa marekani kuwa watu sasa wanaandamana kwasababu matajiri wamerundika mali benki na kuihodhi na huku watu wa kawaida wanateseka na mzunguko unakuwa haupo wa kuzalisha katika nchi au sehemu husika.
Ameruhusu maswali na kujibu swali la muulizaji mmoja aliyesema kuwa hii siyo nchi ya kiislamu na hukumu za kiislamu si rahisi kuzitekeleza ipasavyo, Mwalimu Imrani Atibu amejibu kuwa tusome historia mtume alivyofanya mpaka dola ya uislamu ikasimama tangia akiwa madina mpaka kuhama kwenda maka na kisha kurudi maka akiwa na uwezo kamili wa kusimamisha uislamu maka na madina na mpaka sasa uislamu umeenea dunia nzima.

WhatsApp :+255621870342. Muabudu Mungu mmoja wa Pekee na hana mshirika, Hakuna Mtume aliyetumwa kama Mungu wala Mwana wa Mungu. (Qur'ani) Al Imran 3.31,Yohana 7.16-18. Shetani na kundi lake miongoni mwa wanadamu amejizatiti kuwapotosha watu kupitia shida mbali mbali. Imani kuhusu Mungu mmoja wa pekee ndo suluhisho la kudumu na kuishi na matumaini hapa duniani. Wasiliana nasi upate ushauri na tiba WhatsApp :+255621870342, Email: tibaherbs@gmail.com, +255 762053174
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
CHANGIA MAWAZO YAKO/USHAURI KWA MANUFAA YA JAMII. UNA MAWAZO YAKO NA YANAWEZA KUWA NA MANUFAA YATOE TAFADHALI. KARIBU SANA