Thursday, December 15, 2011

Ubora wa LAA ILAHA ILLA LLAH na matumizi yake-Waadhi na Ust. Faraji Ahmad akiwa Msikiti wa Markaz Kashai(15/12/2011)

Assalam Aleikum.
Nimeona nifikishe nami ujumbe huu alioutoa ndugu yetu katika dini Ust Faraji Ahmad mjini Bukoba baada ya sala ya Magharib.
Alielezea kuhusu umuhimu wa LAA ILAHA ILLALLAH na matumizi yake katika kumtaja ALLAH(SW).
Amesema kuna baadhi ya waislamu wanaitumia visivyo wanapokutana na baada ya salamu mmoja wapo anakanusha bila kuthibitisha upweke wa ALLAH na mwengine anamalizia kwa kuthibitisha upweke wa ALLAH bila kuthibitisha mfano wa kwanza anasema: LAA ILLAHA na wapili anasema ILLA LLAH hii ni kosa na inatakiwa wote waseme LAA ILAHA ILLALLAH.

Ustaz Faraji Abdallah amenukuu Hadithi sahihi hadith li Qudus inayotajwa uzito na ubora wa  LAA ILAHA ILLALLAH
  Kwa muhtasari hadith inaelezea ubora wa  LAA ILAHA ILLALLAH kwa kuchukua vyote vilivyomo katika mbingu saba na ardhi saba bila kumuweka Allah katika vitu hivyo basi ukaweka upande mmoja wa mzani wa kupima uzito na upande mwingine ukaweka  LAA ILAHA ILLALLAH basi  LAA ILAHA ILLALLAH itazidi hivyo vitu vyote vilivyoko katika mbingu saba na ardhi saba kwa uzito. Hii inaonyesha umuhimu wake na akasema Ust Faraji Ahmad kuwa ni bora kutajwa  LAA ILAHA ILLALLAH mara kwa mara kwani hata wakati wa kukata roho kwa mja mwenye kujitahidi kumcha ALLAH akitamka  LAA ILAHA ILLALLAH ikawa ndo kauli yake ya mwisho wakati wa kutoka roho ataingia peponi moja kwa moja.
Tunaomba ALLAH atujalie tumkumbuke mara kwa mara kwani kumtaja ALLAH ni jambo kubwa na lenye kuhuisha imani na kuirejesha katika fikra za Muumba wa kila kitu mara kwa mara.
Kalima hii inakanusha kuwa hakuna Mungu nwingine isipokuwa ALLAH mmoja peke yake na hana mshirika.
Hadithi kuhusu LAA ILAHA ILLALLAH: Li kulli shay'in miftahun wa miftahu al-jannati shahadatu an La ilaha illallah 
  Tafsiri: Kila kitu kina ufunguo na ufunguo wa Pepo ni Kushuhudia kwa kalima ya  LAA ILAHA ILLALLAH
kama una tatizo ya kiafya kama uchawi na majini njoo DSM Kwenye ofisi yetu Vinguguti
Simu

+255712708655/+255713916386

Sheikh wakusoma kisomo cha Ruqya na Dua. Simu.+255 785708655

No comments:

Post a Comment

CHANGIA MAWAZO YAKO/USHAURI KWA MANUFAA YA JAMII. UNA MAWAZO YAKO NA YANAWEZA KUWA NA MANUFAA YATOE TAFADHALI. KARIBU SANA