- Kutochana ndevu mbele ya watu
- Kutoshika shika ndevu mbele ya watu
- Kutochokonoa meno mbele ya watu
- Kutoweka vidole puani mbele ya watu
- Kutokata kucha mbele ya watu
- Kutosimamia watu waliokaa wakifanya mambo yao
- Kutolala ndani ya watu waliokaa
- Kutokaa bila kulala kati ya watu waliolala
- Kutonyoshea watu au mtu kidole akiwa mbali au karibu hata kama unamuongelea vizuri
- Kutolazimisha katika kuomba yaani kugagania kuomba
- Kutofanya urafiki na mtu muongo
- Kutojifanya rafiki wa tajiri asiyekusaidia lolote hata ukiwa na shida
- Kutokaa vijiweni au karibu na njia ila ukilazimika kukaa chunga haki zake kama kuinamisha macho, kuhamrisha mema na kuondoa maudhi kwa watu
- Kutotaniana na watoto na watu walioko chini yako kuzidi kiwango cha kawaida
- Kutorithisha mali zako na bado uko hai:mfano: kugawa nyumba kwa mwanamke kuwa ni yake, mashamba, n.k
- Kutodhihirisha hali mbaya kiuchumi waziwazi kwa mwanamke wako bila ulazima wa kufanya hivyo.
- Kutofanya mali kuwa na thamani kuliko wewe. mfano: kuna watu wanafikia hatua kujidhalilisha ili wapate pesa kama waimbaji wakiwa uchi, michezo ya kuigiza(Comedy), Mashindano ya kuwania urembo, kumfanyia mpango haramu dada yako au shemeji yako, nk ili azini na mtu mwingine ili mradi umepewa mali, wanawake malaya ili wapate mali wanafanya zinaa kila muda na mtu yoyote.
- Kutotembea kwa magoti
Si rahisi kupata mafunzo haya katika dini nyinginezo, hivyo tujitahidi kuzifanyia kazi kwa vitendo ili tuwe mfano wa kuigwa katika jamii. Insha Allah tujitahidi kusoma dini yetu na kuwafunza jamaa zetu uislam kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment
CHANGIA MAWAZO YAKO/USHAURI KWA MANUFAA YA JAMII. UNA MAWAZO YAKO NA YANAWEZA KUWA NA MANUFAA YATOE TAFADHALI. KARIBU SANA