Sheikh Musa Abeid baada ya sala ya Isha tar.3/12/2011 amewapa nasaha waislam kuwa mstari wa mbele kufuatilia maendeleo ya miradi yao kwani hakuna wakuifuatilia kama si waislamu wenyewe. Amewapata taarifa kuwa tar.4/12/2011 jumapili ni siku maalum ya kufunga mwaka wa masomo wa shule iliyojengwa na waislam wenyewe kwa hali na mali iitwayo Qudusi English Medium Primary School iliyoko eneo la Bukoba mjini Kahororo.
Amewasisitiza waislam kushirikiana katika kuendeleza shule hiyo ya pekee yenye kufundisha masomo ya dini kuanzia chekechea na masomo ya kawaida katika manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera Tanzania.
Pia Sheikh Musa Abeid ameongelea ufanisi uliopatikana mpaka kupata barabara ya kufika shuleni kwa gari kuwa ni jambo la kumshukuru Allah(SW) kwani waislamu wamejitoa muhanga kwa maendeleo yao na vizazi vya baadae na Allah atawalipa kwa juhudi zao.
Pia ameongelea wageni kutoka African Muslim Agency waliokuwa wanatafuta namna ya kuweka miradi ya kijamii katika mkoa wa Kagera, alisema Sheikh tuombe Allah ajalie waweze kutekeleza mipango yoa mizuri kwa ajili ya waislam na kinachotakiwa ni ardhi ya kutosha karibu na manispaa ya Bukoba.
Amewanasihi waislam wawe na subira na wavumiliane na kusahihishane pale penye tatizo bila kugombana na kufanyia fitina kwa kukuza mambo yasiyokuwa na uhakika na wala faida kwa umma wa kiislam

WhatsApp :+255621870342. Muabudu Mungu mmoja wa Pekee na hana mshirika, Hakuna Mtume aliyetumwa kama Mungu wala Mwana wa Mungu. (Qur'ani) Al Imran 3.31,Yohana 7.16-18. Shetani na kundi lake miongoni mwa wanadamu amejizatiti kuwapotosha watu kupitia shida mbali mbali. Imani kuhusu Mungu mmoja wa pekee ndo suluhisho la kudumu na kuishi na matumaini hapa duniani. Wasiliana nasi upate ushauri na tiba WhatsApp :+255621870342, Email: tibaherbs@gmail.com, +255 762053174
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
CHANGIA MAWAZO YAKO/USHAURI KWA MANUFAA YA JAMII. UNA MAWAZO YAKO NA YANAWEZA KUWA NA MANUFAA YATOE TAFADHALI. KARIBU SANA