Tuesday, May 1, 2012

Mwenyezi Mungu ni Mmoja

Mwenyezi Mungu hatasamehe binadamu yoyote atakayemshirikisha katika ibada, hii ina maana inatakiwa kumuabudu yeye peke yake bila kuchanganya kitu au kiumbe chochote katika ibada ya kumuabudu Mwenyezi Mungu. Hii ina maana kuwa watu wote wanaofuata dini ya haki ambayo ndio dini ya maumbile na inaendana na mazingira ya zama zote na dini hii itazidi dini zote hata kama watachukia wenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu.

Kwa hiyo uislamu ndio dini ya haki na itazidi kushinda dini zote na hii ina maana waislamu tujizuie kumshirikisha Mwenyezi Mungu kwani shirika ni dhuluma kubwa sana na Allah(SW) hatamsamehe mshirikina ila akiweza kutubu kabla ya kufa na toba ya kweli ndipo atasamehewa.

Wale ambao hawajabahatika kuwa waislamu basi nawafikishia ujumbe kuwa wafuate dini ya uislamu kwa kukiri kuwa Mwenyezi Mungu ni mmoja na Mtume Muhamad(SW) ni Mjumbe wake aliyetuma kwa ajili ya ulimwengu wote na alifikisha ujumbe kwa wanadamu kama mitume wengine walivyofanya mfano Nabii Musa, issa, Ibrahimu, Nuhu, Yakub, na wengineo.

Kuna Baadhi ya madhehebu ya kikristo wanasema Mungu ni mmoja katika utatu yaani Mungu baba, Mungu mwana na Mungu Roho mtakatifu, hii ni kufuru Mungu ni mmoja tu, hakuzaa wala hakuzaliwa na hakuna kinachomfanana katika vyote alivyoviumba na atakavyoviumba. Yeye huamaua kitu na kukiamrisha kuwa na mara mmoja huwapo kama atakavyokuwa ametaka kuwa basi kinakuwa.

Kuna wanadamu kama nabii  Adamu hana baba wala mama, Bi Hawa hana baba wala mama na alitoka kwenye ubavu wa Adamu na Huzair hajulikani baba wala mama yake, na hawa wote huwezi kuwaita Mungu wala watoto wake wa kuzaa, hata malaika si watoto wake ila ni viumbe miongoni mwa viumbe alivyoumba. kwa hiyo ni kufuru kumuita Yesu(Nabii Issa Bin Mariam) kuwa Mungu mwana kwa sababu eti hana baba. je Nabii Adamu ambaye hakuwa na baba wala mama tunamuitaje? Tafadhali acha kufuru itokayo vinywaji mwenu na Mwenyezi Mungu atawasamehe mkiwa waislamu na kuacha ibada za kiushirikina.

Kwa nini dini ya uislamu ni ya haki kuliko dini zote?

Sababu ni hizi zifuatazo:
Mwenyezi Mungu amesema mwenyewe ndani ya Qur'an tukufu
Ibada za kiislamu zinazuia kushirikisha Mwenyezi Mungu
Waislam tunafanya ibada bila kuimba wala kukaa kwenye viti na hatuvai viatu msikitini na kuchanganyikana na wanawake mchanganyiko wa kuhatarisha hulka njema ya waumini wakiwa kwenye ibada
Stara ya mavazi ni ya kufunuka mihili kama wachamungu na watawa wa kale wote walikuwa wanavaa nguo za stara
Viongozi wa za kikristo wanavaa kofia na makanzu, masister wanavaa vitambaa na nguo ndefu za stara kama waislamu wanavyoagizwa.
Waislamu wote wanafundishwa ni bora kuvaa kofia na makanzu kama mavazi ya kiucha Mungu, je mbona waumini wa kikristo wanazuiliwa kuvaa kanzu na kofia kanisani na hali mapadri, maaskofu, makardinari na maaskofu wanavaa kofia na makanzu? Hii inaonyesha kuwa uislamu unaamrisha mavazi kwa kila muislamu ya kiucha Mungu na inaonyesha ukweli wa dini hii ya maumbile.
Kuna mafundisho ya Mtume(SAW) yanayofundisha namna ya kuzika muislamu akifa, kufungisha ndoa ya halali, mtoto akizaliwa namna gani ahudumiwe, kutozini kabla ya ndoa na baada ya ndoa, madhara ya pombe na kutokula nguruwe na madhara ya kamali na riba, la kushangaza huwezi kuona maelekezo ya wazi kwa dini za kikristo ila utaona vitabu vinavyoruhusu kula riba, kunywa pombe bila kulewa na kufuga nguruwe kwa wingi. Jambo moja la kusikitisha watu wanakaa kwenye zinaa mpaka wanazeeka na katika uzee wao wanafungishwa ndoa na mapadri pamoja na wachungaji kiurahisi na siku hizi ni jambo la kawaida ndoa nyingi zinafungwa kwa mtindo huu wa kuruhusu zinaa kwa miaka kadhaa na baadaye kanisa linabariki watu wakiisha ichoka zinaa wanabarikiwa rasmi uzeeni au muda watakao amua.

Sasa kanisa la Anglikani limeruhusu kufunga ndoa mwanaume kwa mwanaume na kanisa linabariki ndoa hizi tumeshuhudia uingereza na kwingineko mambo haya yanafanyika wazi na kanisa linabariki ndoa hizi, uislamu unakemea na hauruhusu tendo hili na kuruhusu muislamu kufanya hivyo sembuse kufunga ndoa!!!

Yesu na Musa walifunga na Biblia inasema kufunga bila kula chochote lakini wakristo wanasema ule kidogo usishibe na wengine wanasema uache unachokitaka sana mfano kama unataka nyama sana usile nyama siku hiyo utakuwa umefunga, je mbona Yesu au Musa walifunga siku kadhaa bila kula chochote mchana na hakuna ruhusa ya kufunga nusu nusu katika biblia nzima hii inaonyesha kuwa wanafuata mafundisho yao na wanaacha mfundisho ya kweli ya Mwenyezi Mungu. ndugu msomaji acha ushabiki na kurithi dini fuata ukweli na uislamu unaonyesha kwa hoja kidogo hizi nilizotowa hapo juu kuwa ni dini ya kweli na aliyechelewa aamuke leo na aingie katika uislamu mzimamzima ili afuate dini ya kweli na ya haki.

No comments:

Post a Comment

CHANGIA MAWAZO YAKO/USHAURI KWA MANUFAA YA JAMII. UNA MAWAZO YAKO NA YANAWEZA KUWA NA MANUFAA YATOE TAFADHALI. KARIBU SANA