Friday, May 11, 2012

Funguo katika mambo ya Kheri-Sheikh Musa Abeid Kashai markaz Bukoba

Tarehe 10/5/2012 Sheikh Musa Abed Imam wa msikiti wa Markaz kashai Bukoba Tanzania aliwapa nasaha waislamu wanaoswalia katika Msikiti huo kuhusu kuazimisha baadhi ya siku za kishirikina zinazotambuliwa kama sikukuu katika nchi mbali mbali ikiwemo Tanzania.

Baada ya hapo kwa ufupi alitoa waadhi kuhusu funguo za mambo ya kheri ili waislamu wazijue hizo funguo na wazitumie kuelekea katika kheri Insha Allah.

Funguo katika mambo ya kheri ni hizi:

Ufunguo wa pepo ni Laa  Illaha Illa  llah
Ufunguo wa Riziq ni kuomba maghfirah na kujishughulisha kufanya kazi
Ufunguo wa kuongezewa na Allah ni kushukuru Allah
Ufunguo wa heshima ni Kumcha Allah na kufuata mafundisho ya Mtume(SAW)
Ufunguo wa Swala ni Twahara
Ufunguo wa Hija ni Kuhirimia nia ya Hija
Ufunguo wa taufiq ni hofu na shauku
Ufunguo wa Nusura ni subira

Pia Sheikh Musa Abed aligusia funguo katika mambo ya shari:
Ufunguo wa maovu ni pombe
Ufunguo wa zinaa ni mziki
Ufunguo wa udhalili ni uzembe
Ufunguo wa moto ni shirki
Ufunguo wa fitina ni uongo

No comments:

Post a Comment

CHANGIA MAWAZO YAKO/USHAURI KWA MANUFAA YA JAMII. UNA MAWAZO YAKO NA YANAWEZA KUWA NA MANUFAA YATOE TAFADHALI. KARIBU SANA