Thursday, April 26, 2012

Ushirikina wa nyota na hukumu yake: Na Sheikh Musa Abeid wa Msikiti wa Markaz Kashai

Sheikh Musa Abeid aliwambia waislamu kuwa kuabudu nyota na kuamini nyota za kiutabiri ni shirki kama shirki nyimgine na ikienda mbali zaidi inakuwa ni uchawi.

Sheikh Musa Abeid amesema kazi ya Nyota za angani ni tatu kwa mujibu wa Qur'an hasa katika Suratil Li Mulki na Assafaati:

Kupamba mbingu ya Karibu
Kushambulia mashaytwani yenye mbawa za kuelea angani pindi yakikaribia anga za juu
Kuongeza wasafiri wa nchi kavu  na baharini yaani ni kama dira kwa wanajimu na watu wenye kufuatilia tabia za baadhi ya nyota.

Kwa hiyo ushirikina ni jambo baya na dhambi kubwa na wachawi hukumu yao ni kukatwa kichwa na hii inaashiria kuwa uchawi na ushirikina ni dhambi kubwa, tumtegemee Allah(SW) kama mlinzi na tumche yeye peke yake na yeye ameahidi kutulinda wa wachawi na sheitani muovu.

No comments:

Post a Comment

CHANGIA MAWAZO YAKO/USHAURI KWA MANUFAA YA JAMII. UNA MAWAZO YAKO NA YANAWEZA KUWA NA MANUFAA YATOE TAFADHALI. KARIBU SANA