Nimepokea taarifa kutoka kwa wanafunzi mbalimbali wa Kashai Sekondari wakilalamika kuhusu manyanyaso ya kidini
1. Mwalimu mmoja wa kike aliwaadhibu wanafunzi wa kiislamu kwa kosa la kusimama pamoja. na kuonywa vikali kwamba hairuhusiwi waislamu kusimama pamoja kama kikundi hata kama wanakunywa uji
2.Mnamo tarehe 23/4/2012 asubuhi saa 8.00 wanafunzi wawili wa kiislamu walitolewa mbele ya wanafunzi wenzao wakaamrishwa wakate jalabibi hadi tai zionekane. Jua kuwa kufunika mikono kwa mwanamke au msichana ni stara kwa waislamu kwa mujibu wa imani yao, hii ina maana wakikata jalabibi mikono itakuwa nje kwani shati za shule ni mikono mifupi
MKUU WA SHULE KASHAI KASHAI SECONDARI
Kulingana na taarifa zilizoelezwa hapo juu yaonekana hayo yote unayaona ni kawaida na hali ya kuwa ni unyanyasaji wa waziwazi kwani kulingana na takwimu ya wanafunzi uliyo nayo wanafunzi wa kikristo ndo wengi takribani robo tatu ya shule. Mbona wakristo hawajakatazwa kusimama peke yao? naomba jibu
PILI
Kulingana na sheria ya dini ya kiislamu msichana haruhusiwi kuonekana mikono yake na serikali imesharuhusu
Vipi unsimamia kauli kwamba wanafunzi wakate Skafu ili Tai zionekane na hali ya kuwa mashati ni ya mikono mifupi?
Mbona hujamtoa Mkiristo aliyevaa kimini? Mbona ni wengi tu?
Huo ni unyanyasaji wa waziwazi na sasa nimekupa taarifa na mwalimu namfahamu jina ila nimemuhifadhi ili ajirekebishe
Umeshaonesha unyasaji wa Tai ndani ya Jalabibi tumekuvumilia, bado unataka wakate nguo!
MWISHO
1. Tunaomba utueleze kama una serikali yako tofauti na serikali ya Tanzania ili tujue
2. Unyanyasaji huo usiporekebikatutachukua sheria dhidi ya ubguzi wa kiimani
Nakutakia utendaji mwema wa kazi na uadilifu bila kutawaliwa na imani ya kidini moyoni mwako

WhatsApp :+255621870342. Muabudu Mungu mmoja wa Pekee na hana mshirika, Hakuna Mtume aliyetumwa kama Mungu wala Mwana wa Mungu. (Qur'ani) Al Imran 3.31,Yohana 7.16-18. Shetani na kundi lake miongoni mwa wanadamu amejizatiti kuwapotosha watu kupitia shida mbali mbali. Imani kuhusu Mungu mmoja wa pekee ndo suluhisho la kudumu na kuishi na matumaini hapa duniani. Wasiliana nasi upate ushauri na tiba WhatsApp :+255621870342, Email: tibaherbs@gmail.com, +255 762053174
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kweli inasikitisha kuona katika Tanzania ya sasa kuna watu wanadekeza ubaguzi wa kidini, hii ni kinyume na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mtu yoyote wa cheo chochote nchini haruhusiwi kukiuka katiba ya nchi na akienda kinyume na katiba basi lazima sheria ichukue mkondo wake. Hii Kashai Secondari iko wapi nchini Tanzania na hawa walimu ni watanzania halali na wazalendo?
ReplyDelete