Baada ya sala ya ishah mwalimu Twaibu Athumani ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Qudus English Medium Primary School na mwalimu wa masomo ya dini Markaz ya Kashai mjini Bukoba ametoa mawaidha kuhusu matumizi ya wakati baada ya kusalisha sala ya ishah.
Amenukuu aya za Qur'an na Hadith za Mtume Muhamad(SAW) kuhusu waja wa mwenyezimungu wema na sifa zao kama kusali kwa muda na kuzingatia sala zao, kuhifadhi tupu zao, kupuuza sehemu za laghawi na kutumia muda wao kwa mambo ya kheri na kuongea na wajinga kwa salama, kutoa mali kwa ajili ya kutaka radhi za Allah(SW) katika mali zao walizochuma kwa alali, kutubia na kujihesabu nafsi zao kila mara na kufanya ibada za usiku kama sala ya tahajudi.
MwalimuTwaibu Athumani ameendelea kuwakumbusha waislamu katika msikiti wa Kashai Markaz kuhusu masikitiko yanayotokea kwa muislamu kupata hasara katika mambo yake binafsi kama biashara kilimo n.k lakini muislamu huyo huyo hawezi kusikitika kwa kupungukiwa siku katika umri kila kunapokucha na kuangalia ametanguliza nini huko Akhera, je ametanguliza heri au shari? Mpaka akatoa mfano wa mtu anayepima uzito wake kila siku akigundua kuna tofauti hata ya kilo moja ya uzito wake bila kutegemea anajiuliza na kusikitika pamoja na kutafuta sababu ya kupata uzito tofauti siku hiyo, hii inaonyesha wanadamu kutokuwa na umakini kuhusu umri wao kuisha bila heri na amali za kumridhisha Allah(SW), tunapashwa kila siku kusikitika kwa kupoteza kila tarehe bila kujua tumefanya nini cha kumfurahisha Allah?(SW). Tunapashwa tujitahidi sana kuomba istighfar mara 100 kila siku kama alivyokuwa anafanya Mtume(SAW) na kumbuka mtume alikuwa ameisha ambiwa na Allah(SAW) kuwa ni mtu wa peponi lakini alikuwa akifanya istghfar mara 100 kwa siku je wewe na mimi ambao kila saa tunafikiria dunia na kufikiria starehe zake kama mpira, mziki, karata, michezo ya kuigiza, n.k na kusahau kabisa lengo la kuumbwa na huku kila siku umri unakwenda na alama tunaziona zinatuonyesha umri kuondoka kama kuanza kuota ndevu kwa vijana, mvi kwa watu wazima, kungoka meno na kuumwa mgongo kwa watu wazima, sasa hii inatupa taarifa kuwa tumeisha jiandaa saa yoyote malaika wa mauti anaweza akapiga hodi na tuombe kuhairisha mauti ili tufanye mema na kutoa kwa ajili ya Allah lakini itakuwa too late na tutaanza kuwa na imani wakati wa mauti lakini wapi tujuta kwani majuto huja baadaye. Mwalimu Atwibu Athumani ameongelea kuhusu mpira na kupoteza wakati kwenye mpira kiasi kwamba mtu hawezi kutoa sadaka kabla ya kutoa bajeti ya mpira je unapata nini kwenye mipira ya ulaya na hata ya hapa hapa na kuingia ni pesa na muda wa sala unapita na hapo hapo laghawi na mzaha na ushabeki unaingiza maneno machafu na kuharibu murua na tabia njema ya waislamu na kufisha moyo kiasi kwamba mtu hawezi kumsabihi Allah(SW)akiwa kwenye mpirana atafikiria mpira na hata kuanza kutumia simu kuwajulisha marafiki zake na washabiki wenzake kuhusu mpira na matokeo yake na hawezi kuwapigia jamaa na waislamu kuhusu kumcha Allah (SW) iliawe katika waja bora wa kuamrisha mema na kukataza mabaya.
Mwalimu Twaibu Athumani amesema kutoa hata kitu kidogo ni bora kwa sasa kwani Mtume alisema itafika zama hata mtu akitaka kutoa atakosa mtu wa kumpa kwani kila mtu atakuwa tajiri katika siku za mwisho za kukaribia kiyama, kwani sadaka ni muhimu na kulisha maskini pia na mayatima na kuhakikisha kila siku unafanya mema kadiri ya uwezo wako na kuomba Allah(SW) akupe rehema upate mwisho mwema. Mwalimu Twaibu amesema ni muhimu kufanya dhikir kwa kumtaja Allah(SW) kwa dhati kutaja kalima ya Laa ILaha Illa LLAH kadiri ya kurdia angalau mara 200 kwa siku nadhikiri nyinginealizokuwa anafanya Mtume wetu(SAW).

WhatsApp :+255621870342. Muabudu Mungu mmoja wa Pekee na hana mshirika, Hakuna Mtume aliyetumwa kama Mungu wala Mwana wa Mungu. (Qur'ani) Al Imran 3.31,Yohana 7.16-18. Shetani na kundi lake miongoni mwa wanadamu amejizatiti kuwapotosha watu kupitia shida mbali mbali. Imani kuhusu Mungu mmoja wa pekee ndo suluhisho la kudumu na kuishi na matumaini hapa duniani. Wasiliana nasi upate ushauri na tiba WhatsApp :+255621870342, Email: tibaherbs@gmail.com, +255 762053174
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
CHANGIA MAWAZO YAKO/USHAURI KWA MANUFAA YA JAMII. UNA MAWAZO YAKO NA YANAWEZA KUWA NA MANUFAA YATOE TAFADHALI. KARIBU SANA