Tuesday, January 3, 2012

Msiba wa Sheikh Yusufu Ibrahim Rukokerwa

Inna Lillah wainna ileiy rajiuun, sheikh yusufu ibrahimu Rukokerwa amefariki dunia tarehe 3/1/2012 na kuzikwa kitongoji kagabiro kata kasharu. Sheikh Yusufu ameacha watoto 17 na wajukuu 76 wake wawili na ameugua kipindi cha miaka karibu minne.
Katika msiba huu tumejifunza mambo muhimu kutokana na umri wake wa miaka 90 na uongozi katika dini kama sheikh wa Mtaa kwa miaka karibu 25 na imamu wa msikiti kwa muda mrefu. Mawaidha yametolewa na Ustaz Adinani Sudi kutoka Bukoba mjini, na amesema kila nafsi itaonja mauti kwa mujibu wa Qur'an na kila mtu atalipwa kwa mujibu wa amali alizofanya kabla ya kufa kwake. Sheikh Muhamad kassimu kutoka kyenge naye ameongelea kuhusu kumcha Allah(SW) ili kupata radhi za Allah hatuna budi kumcha yeye peke yake.
Kila mwanadamu akiwa hai lazima afanye hesabu ya matendo yake na ajirekebishe kabla ya saa ya kukata roho ili Allah (SW) aweze kumsamehe kwa rehema yake na siyo kukaa bila kufanya amali akategemea kuwa ataombewa dua wakati wa kuzika na kuswaliwa ndipo Allah atamsamehe, hii si kweli bali kila nafsi itabeba mzigo wake wa kheri au wa madhambi na kupata hukumu kwa mujibu wa amali na hii ikiambatana na rehema ya Allah(SW).

No comments:

Post a Comment

CHANGIA MAWAZO YAKO/USHAURI KWA MANUFAA YA JAMII. UNA MAWAZO YAKO NA YANAWEZA KUWA NA MANUFAA YATOE TAFADHALI. KARIBU SANA