Monday, February 13, 2012

Mdilu wa Jimbo la Bukoba Mjini-Sheikh Athumani asititiza Kufuata mafunzo ya Qur'an Na Sunna vilivyo

Mdilu wa Jimbo la Bukoba Mjini atoa changamoto kwa waislamu kuhusu kufuata mafunzo ya uislamu kamili yaani kufuata mafunzo yaliyopo kwenye Qur'an na Hadith za mtume(Sunna) ili kuepuka na matatizo mbalimbali ya kilimwengu kuanzia kwenye familia na jamii kwa ujumla. Matatizo mengi yanayoathiri jamii yasingekuwepo kama sisi wanadamu tungekuwa tunafuata mafunzo ya uislamu vilivyo. Kuanzia matatizo ya kifamilia na kiuchumi yanayotokea kila kukicha na kusababisha maadili kuzidi kuporomoka katika jamii yangekuwa kama historia kama tungekuwa tunafuata maagizo ya Allah(SW) na Sunna za mtume(SAW) vizuri.

Mdilu wa Jimbo Sheikh Athumani akiwa Msikiti wa Markaz Kashai tarehe 12 baada ya Sala ya Magharib alihamasisha uchangiaji wa ujenzi katika Msikiti wa Kashai markaz na waislamu waliokuwepo walichanga ili ujenzi wa sehemu ya kutawadhia usikwame kwani uislamu unasisitiza usafi na udhu unakuwa salama na timilifu utakapopatia udhu sehemu inayofaa na salama. Zoezi hili la kuchangia maendeleo ya uislamu linaendelea kwani maendeleo hayawezi kupatikana bila waislamu kuchangia maendeleo yao na hii itamfanya mchangiaji apate thawabu na hii ni faida hapa duniani na baada ya kufa kwani wema katika uislamu utalipwa siku ya kiyama, sadaka hizi zinasaidia ALLAH (SW) kutuhurumia na kutufutia baadhi ya madhambi yetu tunayoyajua na yale tusiyoyajua, kwa hiyo ndugu waislamu toeni sadaka mara kwa mara ili tupate radhi za Allah(SW).

No comments:

Post a Comment

CHANGIA MAWAZO YAKO/USHAURI KWA MANUFAA YA JAMII. UNA MAWAZO YAKO NA YANAWEZA KUWA NA MANUFAA YATOE TAFADHALI. KARIBU SANA