Wednesday, November 14, 2012

Haji Jafar Bwanika-Kifo na Mazishi yake

Al-Haji Sheikh Jafar  Bwanika amefariki tar 9/11/2012 kuamkia Ijumaa akiwa Hospitalini DSM alikokuwa amekwenda kwa matibabu zaidi.

Sheikh Jafar alikuwa ni kiongozi wa dini na pia kiongozi wa jamii kwani katika umri wake wa takribani miaka 74 aliisha kuwa kiongozi wa serikali kisiasa na kiongozi wa ushirika. Akiwa ni Imamu na Sheikh mwenye bidii ya kuhakikisha dini inaendelezwa katika eneo la Kamachumu na mkoani Kagera kwa ujumla ameweza kuwa na mahusiano na watu wa dini zote katika Tanzania. Hii imethibitishwa katka mazishi yake ambayo yamehudhuriwa na watu mbali mbali kutoka mikoa ya DSM, Mwanza, Singida, n.k. watu waliohudhuria pale walikuwa wengi wakiwemo Masheikh wakubwa kama Sheikh Mustafa Kharidi Kutoka Katoro, Sheikh WALID ALIHAD OMARY kutoka DSM, Sheik Haruna Kichwabuta Bukoba Manispaa, Sheikh Maulana Bukoba, n.k.

Waislamu, ndugu na jamaa wote waliitikia kuja kumuombea dua marehemu na vijana wadogo kutoka ibwera wakiwa na mwalimu wao Muhammad waliongoza dua hiyo.

Hapa ni wakati wa kumsomea dua Marehemu Sheikh Jafar Bwanika nyumbani kwake kijiji Bushagara Kamachumu. Dua ilisomwa tarehe 14/11/2012